Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya barua ya shukrani ya Ayatollah Arafi kwa Imam Khamenei ni kama ifuatavyo:
Bismillahir Rahmanir Rahim
Kumuelekea mtukufu Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi)
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kwa heshima, salamu na maamkizi
Ninajiona kuwa ni mwenye wadhifa kutoa shukrani kutokana na chaposho la hawza na ujumbe wenu wa kihistoria na muhimu uliotolewa kwa ajili ya tukio hilo la kihistoria na kielimu katika kumbukumbu ya miaka mia tangia kuasisiwa upya kwa Hawza ya Qom na kwa kumuenzi Ayatollah al-Udhma Hairi (ra), ambapo: Kwanza, napenda kuwasilisha shukrani nyingi na za dhati za wanahawza wote kwa hadhira tukufu yenu; na pili, natangaza upya ahadi na kiaga cha wanahawza wote kwa ngazi, tabaka na taasisi mbalimbali za hawza, kwa ajili ya kujitolea katika kufuatilia madai na miongozo ya mheshimiwa mtukufu.
Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Azimio la “Hawza inayosonga mbele na iliyo kileleni”" lililotolewa na nyinyi kwenye tukio hili kubwa la hawza, limeipa hari mpya hawza, wanafunzi na wanazuoni vijana, pamoja na mchakato mzima wa mageuzi ya hawza, na kwa mujibu wa fikra ya asili na yenye ufanisi ya kiongozi wa hawza, limeielekeza hawza kuelekea upeo ulio wazi na wa kistaarabu, na limekuwa mwanzo wa hatua mpya na ya kihistoria katika mabadiliko ya Hawza ya Qom na hawza nyengine kwa ujumla, katika mwanzoni mwa karne ya kumi na tano ya Hijria/Shamsi.
Ahadi na kiaga cha hawza na mihimili yake yote ni kwamba Hawza tukufu na yenye mafanikio ya Qom na hawza nyengine, kuwa na maarifa ya kina kuhusu mwanadamu, dunia na kijana wa zama hizi, na mtazamo wa kina kuhusu mahitaji ya Mapinduzi na mfumo wa Kiislamu, pamoja na kutambua upya maeneo ya nguvu na udhaifu na mapungufu yaliyopo, na kwa kuamsha uwezo wa hawza kwa kiwango cha juu kabisa, Hawza zitaendeleza juhudi za kutekeleza azimio hili. Hili litafanyika kupitia uchambuzi na ufafanuzi, kukuza muelekeo wa azimio hili, kulipangilia kwa njia ya kivitendo na kupanga utekelezaji wake, na kulijumuisha ndani ya mipango mipya ya muda wa kati na muda mrefu wa mageuzi ya hawza. Kwa uwezo wake wote, hawza itajiandaa na kuchukua hatua ili kuendeleza njia iliyoanza ya mageuzi na ufanisi wa hawza.
Katika hili, tutanufaika na urithi wa watu wema waliotangulia, pamoja na miongozo ya Imam Khomeini (ra), marjaa wa kidini wakubwa, na pia miongozo na madai yenu ya kihistoria katika miongo ya hivi karibuni, kwa ajili ya kutekeleza mihimili iliyosisitizwa ndani ya azimio la hawza.
Tuna matumaini kuwa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kwa mtazamo wa Imam Mahdi (arwaḥuna fidah), pamoja na umoja, mshikamano na ushirikiano wa wanahawza wote, hasa wanafunzi, wanazuoni na walimu vijana, na taasisi mbalimbali za hawza, njia ya ustawi na utumishi wa hawza itaendelea. Tunalo tumaini kamili kuwa uongozi na baraka zenu, kama ilivyokuwa siku zote, vitakuwa mwongozo na msaada wa hawza katika njia hii.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ajaalie afya, utukufu na ushindi wa kimungu kwa kiongozi huyo wa thamani, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, taifa la Iran, Umma wa Kiislamu na mrengo wa muqawama.
Kivuli chako kilicho juu daima kisalie kuwa juu.
Alireza Arafi
Mkurugenzi (Mudir) wa Hawza Irani
Maoni yako